Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litapiga kura leo Ijumaa asubuhi juu ya azimio la kuchelewesha kurejeshwa kwa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran, inayoshutumiwa na Ufaransa, Ujerumani na Uingereza kwa kukiuka ahadi zake za nyuklia.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa hakuna azimio litapitishwa kufikia mwisho wa mwezi, vikwazo dhidi ya Tehran vitarejeshwa moja kwa moja, chini ya utaratibu uliowekwa katika Mkataba wa Vienna na kuchochewa na nchi tatu za Ulaya

Urusi na China zimeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuipigia kura rasimu ya azimio la kuchelewesha kwa miezi sita vikwazo dhidi ya Iran.

Vikwanzo vyote vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran vinatazamiwa kuanzishwa tena leo Ijumaa usiku baada ya Ufaransa, Uingereza na Ujerumani kuchochea mchakato wa siku 30, zikiituhumu Tehran kwa kukiuka mkataba wa 2015 na mataifa hayo yenye nguvu kiuchumi duniani, juu ya shughuli zake za nyuklia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *