#HABARI: Naibu Waziri wa Viwanda Dennis Londo amesema itaendelea kuboresha sera na kuimarisha miundombinu rafiki ikiwemo ya barabara ili kufungua fursa nyingi za uwekezaji ambazo zitaendelea kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa kuwekeza mazingira wezeshi ya kibiashara kwa wawekezaji.
Akizungunza katika uzinduzi wa kiwanda kipya cha magodoro cha Federal wilayani Mkuranga mkoani Pwani, Mhe. Londo amesema hayo ni maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia dira ya maendeleo ya nchi 2020-50 unaolenga kujenga uchumi jumuishi wa kisasa unaopigania viwanda, teknolojia na ubunifu na kuhakikisha maendeleo jumuishi yanawanufaisha wengi likiwemo kundi la vijana.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe Wanu Hafidh Ameir ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda na waajiri kuendelea kushirikiana na taasisi za elimu na mafunzo kwa kutoa fursa za mafunzo kwa vitendo na kushiriki katika uandaaji wa mitaala kwani ushirikiano ni muhimu katika kuandaa rasilimali watu wenye umahiri kuongeza tija ya uzalishaji na kuimarisha ushindani katika masoko ya ndani ya Kimataifa.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge alipongeza hatua ya uwekezaji huo ambao umeongeza idadi ya uwepo wa viwanda 286 wilayani Mkuranga ambapo kiwanda hicho ni kikubwa hivyo uwekezaji huo utawezesha Mkuranga na Mkoa wa Pwani kuongeza mapato na uchumi wa mkoa huo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.