#HABARI: Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, ameitaka Serikali pamoja na wadau wa sekta binafsi kuhakikisha maboresho ya mfumo wa kodi yanatekelezwa kwa awamu tatu za muda mfupi, wa kati na mrefu ili kuleta matokeo ya haraka na endelevu.
Ameeleza haya wakati akipokea ripoti ya Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi na kusema kwamba kuna haja ya kufanya uchambuzi wa kina na kuanza utekelezaji mara moja kwa maeneo ambayo hayahitaji mjadala mrefu, ili kuharakisha mageuzi yanayolenga kujenga mfumo imara wa kodi nchini, na kwamba dhamira yake ni kuona msingi thabiti unawekwa wakati wa uongozi wake, ili kuhakikisha dira ya maendeleo ya taifa inatekelezeka kwa ufanisi katika siku zijazo.
Rais Samia amewataka watendaji wa Serikali, wafanyabiashara na wajasiriamali kushirikiana katika mchakato wa mabadiliko hayo, akieleza kuwa ni kawaida kwa mageuzi kuambatana na changamoto na usumbufu wa awali.
“Kwa muda mrefu tumekuwa tukitumia mfumo wa kodi wa zamani kwa takribani miaka 35, hivyo kufanya mabadiliko ni sawa na kunyoosha mkono uliokuwa umekunjamana, lazima kutakuwa na maumivu”
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.