#HABARI: Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala, chini ya Mwenyekiti wake Ndg. Sabry Shariff, imefanya kikao cha kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa majukumu ya elimu, malezi, na afya.

Mgeni rasmi katika baraza hilo, Katibu wa Waziri Wilaya ya Ilala Ndg. Mtiti Jirabi Mbassa, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya walimu na wazazi mashuleni ili kuimarisha maadili na mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi, huku akihimiza vikao vya mara kwa mara kati ya pande hizo mbili.

Aidha, kikao hicho kimejadili mikakati ya kuongeza wanachama kupitia mfumo wa kielektroniki na kufanya tathmini ya uchaguzi wa serikali kuu wa mwaka 2025 kuelekea uchaguzi wa chama mwaka 2027.

Wajumbe walipata fursa ya kupambanua masuala ya utamaduni na mazingira kwa uyakinifu, ambapo mkutano huo ulihitimishwa kwa washiriki kujumuika pamoja katika chakula cha Iftar ikiwa ni ishara ya upendo na mshikamano.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *