#HABARI: Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), imeanza zoezi la upandaji miti katika msitu wa Machang’anja wilayani Ruangwa baada ya hekta 400 kati ya 1,000 kuharibiwa na shughuli za binadamu, ikiwemo kilimo cha ufuta.

Mhifadhi Misitu wa Wilaya, SCO Elibariki Lagwen, amebainisha kuwa zaidi ya miti 700,000 imepandwa wilayani humo katika kipindi cha miaka mitano, ikiwemo maeneo ya shule, ili kurejesha uasili wa msitu huo na kulinda rasilimali kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa, Solomoni Masanja, amepongeza ushirikiano uliopo kati ya TFS na wananchi katika uhifadhi wa mazingira, huku walimu na wanafunzi wakieleza kuwa upandaji huo una tija kubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Hatua hiyo inalenga kukomesha uharibifu uliokithiri na kuhakikisha wilaya hiyo inabaki na uoto wa asili unaovutia mvua na kulinda vyanzo vya maji kwa ajili ya ustawi wa jamii.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *