Rais Masoud Pezeshkian wa Iran ametuma ujumbe na kuandika kuwa: Mashambulizi dhidi ya miundo msingi ya nishati ya Iran yana taathira ambazo ukubwa wake utaitatiza dunia nzima.

Rais Pezeshkian ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba: Ninalaani vikali mashambulizi dhidi ya miundo mbinu ya nishati ya Iran.

Hatua za kichokozi kama hizi hazitakuwa na manufaa kwa audi Mzayuni, Marekani na waungaji mkono wao bali zitaifanya hali ya mambo kuwa mbaya zaidi na kusababisha taathira zisizoweza kudhibitiwa zinazoweza kuiyumbisha dunia nzima. 

Mapema jana Israel na Marekani zilishambulia baadhi ya maeneo ya visima vya gesi vya Pars-Kusini vinavyopatikana kusini mwa Iran katika siku ya 19 ya vita vilivyoanzishwa na tawala mbili hizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Iran imejibu uchokozi huo kwa kuchambulia vituo vikubwa zaidi vya kusalisha gesi katika nchi za Saudi Arabia na Qatar ambavyo vinamilikiwa na makampuni ya Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *