
Shirika la AFP limeripoti kusikika kwa milipuko na kuona moshi mkubwa ukifuka kutoka maeneo matatu katika eneo la Sanaa, katika shambulizi hilo la hivi punde zaidi la kulipiza kisasi tangu kundi hilo lilipoanza kuilenga Israel kufuatia vita vya Gaza.
Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kundi hilo la Houthi vimeripoti kuwa vikosi vya Israel vilishambulia maeneo kadhaa yanayohusishwa na kundi hilo mjini humo na kuonya kutokea kwa mashambulizi zaidi.
Baadaye, jeshi la Israel lilisema kuwa kombora lililorushwa kutoka Yemen lilinaswa, huku ving’ora vikilia katikati mwa Israel.