#HABARI: Simanzi nzito imetanda katika Kijiji cha Buruga, wilayani Serengeti, kufuatia vifo vya ndugu watatu wa familia moja baada ya kunywa dawa ya kienyeji iliyotokana na magome ya miti shamba.

Waliopoteza maisha ni Kashi Joseph (52), Marco Machota (51), na Devota Nyamhanga (58), ambao walikunywa mchanganyiko huo wakiamini ni dawa ya kutibu nyongo na kuongeza hamu ya kula, kabla ya kuanza kuugua na kufariki dunia muda mfupi baadaye.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, SACP Pius Lutumo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku uchunguzi wa kina ukianza kubaini aina ya miti hiyo na kiini cha vifo hivyo.

Diwani wa Kata ya Uwanja wa Ndege, Matoke Michael, amelaani tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha kutumia dawa za asili ambazo hazijathibitishwa na mamlaka za afya ili kuepuka majanga yanayoweza kuzuilika ndani ya jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *