
Zaidi ya wanajihadi wa kiislamu 100 wameachiwa huru hivi karibuni na mamlaka za Mali, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya wao kusitisha mashambulio dhidi ya misafara ya malori ya mafuta, mashambulizi ambayo yametatiza upatikanaji wa nishati hiyo kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tangu mwezi Septemba, kundi moja la wanajihadi wa kiislamu wenye uhusiano na mtandao wa kigaidi duniani, Al Qaeda, limekuwa likishambulia misafara ya malori ya mafuta, hali ambayo imefanya shughuli kwenye jiji la Bamako kusimama kutokana na uhaba wa mafuta.
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani vilivyozungumza na shirika la habari la AFP, vilithibitisha kuachiwa kwa wanajihadi zaidi ya 100 kwa kubadilishana na kufunguliwa kwa njia kuu za kibiashara ambazo zimekuwa zikitumiwa na malori kupitisha mafuta kwenda Bamako.
Kwa mujibu wa viongozi wa Bamako, makubaliano haya yatasalia hadi pale sherehe za Eid al Adha maarufu kama Tabaski kwenye ukanda huo, zitakapomalizika mwishoni mwa mwezi Mei.