RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) David Nchimbi Ikulu Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) itaendelea kushirikiana na TTCL katika kuimarisha huduma za mawasiliano Zanzibar kupitia huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, David Nchimbi amemshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa ushirikiano unaoendelea kati ya shirika hilo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha huduma za mawasiliano. SOMA: TTCL waja kivingine huduma intaneti

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *