Chad imeanza kutekeleza mpango wa dharura wa kuwahamisha wakimbizi toka kwenye mpaka wake na Sudan, kufuatia mfululizo wa mashambulizi ya hivi karibuni wakati huu pia wanajeshi zaidi wakitumwa kwenye eneo hilo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Chad, hatua hii inalipa jeshi lake uwezo wa kujilinda kufuatia shambulio la droni ambalo lilirushwa kutoka Sudan.

Tayari Chad imewahamisha karibia wakimbizi 2,300 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto ambao wamepelekwa katika maeneo ya ndani zaidi kutoka kwenye mpaka.

Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby aliagiza kuhamishwa kwa wakimbizi hao baada ya shambulio hilo la droni kusababisha vifo vya watu 17, Sudan ikituhumiwa kuhusika.

Kando na kuwahamisha, Chad pia imeongeza usalama kwenye mpaka wake na Sudan, kukiwa na hofu kwamba inaweza kuwatuma wanajeshi katika ardhi ya Sudan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *