Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema Serikali imeanza mazungumzo na UNESCO pamoja na uongozi wa Kampuni Mama inayomiliki Faceebok, Instagram na WhatsApp (META) ili Lugha ya Kiswahili itambulike rasmi kwenye Majukwaa ya Kimtandao na kuwezesha Vijana wanaotengeneza maudhui kwa lugha hiyo walipwe malipo makubwa kulingana na kazi zao.

Amesema hayo wakati wa kongamano la tano la Idhaa za Kiswahili duniani linaloendelea jijini Arusha lleo Machi 24, 2026 na kubainisha kuwa licha ya maudhui ya Lugha ya Kiswahili kuwa mazuri na kupata watazamaji wengi warushaji wanalipwa kidogo kutokana na lugha hiyo kutokuwa rasmi kwenye majukwaa ya mitandao hiyo ukilinganisha na Kiingereza,

“leo hii unamkuta mtu wa Tanzania ana followers (wafuasi) zaidi ya milioni tatu, akipost wanaotazama ni wengi ila hapati fedha kupitia Instagram, Facebook, TikTok hawawalipi kwasababu Kiswahili bado Watu wa META na wenye platform ya mitandao duniani hawajakitambua kama lugha rasmi” amssisitiza Makonda.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *