Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limetoa wito wa “kujizuia” muda mfupi baada ya Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran kuripoti shambulio lingine, ambalo halikusababisha uharibifu wowote, kwenye kituo cha nyuklia cha kiraia cha Bushehr.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

“Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi anarudia wito wake wa pande husika kujizuia ili kuepuka hatari yoyote kwa usalama wa nyuklia wakati wa migogoro,” shirika la Umoja wa Mataifa limesema katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa X. IAEA imesema kwamba Iran imeifahamisha kwamba “kombora lingine lilishambulia majengo” ya kituo cha nyuklia cha Bushehr siku ya Jumanne.

Kituo hiki, kinachopatikana kusini mwa Iran, tayari kililengwa wiki iliyopita na “kombora,” ambalo halikusababisha uharibifu wowote kwa miundombinu au kusababisha majeraha kwa raia, IAEA imesema. Urusi, ambayo inaajiri wataalamu katika kiwanda hicho, ililaani shambulizi hilo kama “lisilowajibika.”

Kituo  nyuklia cha Bushehr, pekee kinachofanya kazi nchini Iran, kina uwezo wa uzalishaji wa megawati 1,000, ambazoz inawakilisha sehemu ndogo tu ya mahitaji ya umeme ya nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *