SERIKALI Mkoani Geita imewahakikishia wananchi kuwa chanjo ya kinga dhidi ya Polio ni salama na imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Wizara ya Afya nchini.

Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa kampeni ya chanjo hiyo katika Manispaa ya Geita, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Hashimu Komba, amesema serikali imejipanga kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo hiyo kwa usalama na ufanisi.

Amesisitiza kuwa licha ya kuwepo kwa taarifa za upotoshaji zinazojitokeza wakati wa kampeni za chanjo, jamii inapaswa kuzipuuza na kuendelea kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo muhimu la kulinda afya za watoto. SOMA: Watoto milioni moja kupatiwa chanjo ya polio Geita

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *