
Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa umetangaza siku ya Jumatano, Machi 25, biashara ya utumwa wa Waafrika kama uhalifu mbaya zaidi dhidi ya ubinadamu, vita vinavyoongozwa na Ghana, ambayo inatumaini kufungua njia ya kuomba msamaha na haki.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Licha ya kutoridhishwa na Marekani na nchi za Ulaya, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulitangaza, siku ya Jumatano, biashara ya utumwa Afrika kama uhalifu mbaya zaidi dhidi ya ubinadamu.
Akiwa mtetezi mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) wa fidia zinazohusiana na biashara ya utumwa ya kuvuka Atlantiki, Rais wa Ghana John Mahama alisafiri hadi New York kuendeleza nakala hii isiyofungamana, ambayo hata hivyo anaiona kuwa “ya kihistoria.” “Leo, tumekusanyika kwa dhati na mshikamano kutangaza ukweli na kuendelea na njia ya kuelekea uponyaji na kurejesha haki,” alisema katika siku hiyo ya maadimisho ya mateso ya wanaume, wanawake na watoto milioni 13 ambao walifaniwa udhalimu kwa kipindi cha miaka 400.
Azimio hilo, lililopitishwa kwa kura 123 zilizounga mkono, 3 zilizopinga (Marekani, Israel, Argentina), na 52 zilizojizuia (ikiwa ni pamoja na Uingereza na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya), linatangaza “biashara ya utumwa na utumwa wa rangi wa Waafrika” kama “uhalifu mbaya zaidi dhidi ya ubinadamu,” likilaani “dhuluma hii isiyo ya kibinadamu na inayoendelea kufanywa dhidi ya ubinadamu.” Kwa kweli, hili lilikuwa hoja kuu ya mzozo: baadhi walibishana kwamba hakuwezi kuwa na uongozi wowote kati ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na kwa hivyo haungeweza kupiga kura ya kuunga mkono, anaripoti mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten.
Swali la fidia katikati ya mijadala
Licha ya kupitishwa kwa azimio hilo, mjadala huo haujaisha. Kwa baadhi, kura hii inasalia kuwa ya mfano na haihakikishi fidia halisi, kama mtafiti na mwanaharakati Obadele Kambon, kutoka Chuo Kikuu cha Ghana, alivyomweleza Christina Okello wa RFI.
Hili si swali la zamani tu; ni ukweli unaoendelea kushuhudia sasa, ndiyo maana, kwa maoni yangu, mjadala huu unazidi kile tunachokiita kama ishara.
Azimio hilo pia linatoa wito kwa mataifa kushiriki katika mchakato wa haki ili kurekebisha makosa ya zamani. Washington ilidai kwamba nchi za kisasa haziwezi kuwa wanufaika wa fidia kwa waathiriwa wa zamani. Hapo awali, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres aliwasihi wanadiplomasia kuwaheshimu waathiriwa wa biashara ya utumwa ya kuvuka Atlantiki si tu kwa “maneno” yao bali pia kwa “matendo” yao.
Accra, kwa upande wake, inataka hatua madhubuti: ufadhili wa elimu, programu za mafunzo, na usaidizi kwa vijana na wajasiriamali ili kurekebisha ukosefu wa usawa uliorithiwa kutokana na utumwa. Zaidi ya Waafrika milioni 12 walifukuzwa. Na kwa mamlaka ya Ghana, fidia hazizuiliwi na pesa tu.
Kuna kutokuwa na uhakika mwingi kuhusu utekelezaji wa hatua hizo. Huu ni uchambuzi wa Profesa Emmanuel Saboro, mtaalamu wa masuala ya kumbukumbu na utumwa katika Chuo Kikuu cha Cape Coast, Ghana.
Baadhi wanatetea kufutwa kwa deni, kwani Afrika bado inadaiwa pesa na mamlaka za kikoloni—deni lililojengwa kwa sehemu kutokana na utajiri unaotokana na kazi ya Waafrika.
Kipaumbele kingine: urejeshaji wa mabaki ya kitamaduni. Mamilioni ya vipande vilichukuliwa—kutoka Ufalme wa Ashanti, Milki ya Mali, na Ufalme wa Benin. Kwa Accra, vitu hivi si mali tu: vina thamani ya kiroho. Ni sehemu ya historia na utambulisho wa watu wa Afrika.
Kuna baadhi ya mifano. Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Ujerumani ililipa fidia kwa Israel. Lakini katika kesi ya biashara ya watumwa ya kuvuka Atlantiki, jukumu bado linapingwa. Na mjadala huu unasikika haswa nchini Ghana. Kwa ngome na majumba yake, Ghana inabaki kuwa moja ya sehemu kuu za kumbukumbu za historia hii.