
Nchini Sudan Kusini, imepita mwaka mmoja kamili tangu kukamatwa na kuzuiwa nyumbani kwa aliyekuwa Makamu wa kwanza wa rais , Riek Machar.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mwaka mmoja baadaye, Machar bado amezuiwa nyumbani kwake. Amefunguliwa kesi ya uhaini na uhalifu dhidi ya binadamu baada ya vikosi vinavyomuunga mkono kuvamia jeshi la nchi hiyo katika jimbo la Upper Nile.
Machar anakanusha madai dhidi yake, anayosema ni ya kisiasa, huku nchi hiyo ikiendelea kushuhudia utovu wa usalama na kutotekelezwa ipasavyo kwa mkataba wa amani wa mwaka 2018, hali ambayo inatishia kurejesha nchi hiyo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Wafuasi wa Machar, wanamtuhumu rais Salva Kiir, kwa kumfungulia mashtaka ya uongo mpinzani wake, kama njama ya kumzuia kuwania urais.
Sudan Kusini, iliyopata uhuru wake mwaka 2011, baada ya kujitenga na Sudan inatarajiwa kuwa na uchaguzi wake mkuu wa kwanza mwishoni mwa mwaka huu, baada ya kuahirishwa mara mbili.
Hata hivyo, mpaka sasa haijafamika vema iwapo kweli uchaguzi huo utafanyika kutokana na changamoto za kiusalama, maandalizi ya Tume ya Uchaguzi na kutekeleleza baadhi ya vipengele muhimu kwenye mkataba wa amani wa mwaka 2018, ili kuwewezesha uchaguzi huo kuwa huru na haki.