Timu ya Taifa Tanzania, Taifa Stars imepoteza mchezo wa kirafiki maarufu kama FIFA Series kwa bao 1-0 dhidi ya Liechtenstein kutoka Ulaya.

‎Katika mchezo huo ambao umechezwa Uwanja wa Pele, Rwanda Taifa Stars imeshindwa kutumia nafasi ambazo imetengenezwa na kuhukumiwa kwa kosa hilo moja na mechi kumalizika kwa Tanzania kupoteza.

‎Leichtenstein nchi yenye jumla ya watu Elfu 40 nchi nzima inaibuka kidedea baada ya kucheza mechi 13 bila ushindi.

‎Taifa hilo ambalo liko katikati ya Austria na Uswizi kwenye viwango vya ubora wa FIFA inashika nafasi ya 205 kati ya timu 211 huku Tanzania ikishika nafasi ya 110.

‎Ikumbukwe Taifa Stars chini ya Miguel Gamondi mpaka leo haijui ladha ya ushindi kwani ni vipigo na sare.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *