
Wakati wa mkutano mbele ya Baraza la Usalama, Vivian van de Perre, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC ambaye pia anahudumu kama kaimu Mkuu wa MONUSCO, ameomba kwa nchi wanachama uwezo mwingine wa kifedha ili kutimiza kazi iliypewa kikosi hicho mwezi Desemba mwaka uliyopita.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten
Wakati wa mkutano kuhusu hali mashariki mwa DRC mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi, Machi 26, huko New York, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini DRC alibainisha kwamba vurugu na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika eneo hilo lazima zikome. Katika hotuba yake, Vivian van de Perre pia alitaka ufikiaji wa kibinadamu udumishwe na ahadi za kidiplomasia zilizotolewa katika suala hili zitekelezwe haraka.
Kaimu Mkuu wa MONUSCO hatimaye ameomba kuongezwa kwa bajeti ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC ili kuajiri na kupeleka wanajeshi wapya kusaidia utaratibu wa kusitisha mapigano, kama Baraza la Usalama lilivyomwomba kufanya mwezi Desemba waka uliyopita.
Kuongezwa kwa wanajeshi baada ya kupunguzwa kwa 25%
Ingawa MONUSCO imetumia teknolojia mpya ili kuwalinda raia kwa ufanisi zaidi na imejipanga upya katika maeneo ambayo yana athari kubwa zaidi, kwa mfano, kwa kuunda vituo sita vya watu kuhamia huko Ituri, kikosi hicho kwa sasa hakina rasilimali za kutosha kutekeleza kazi hii, alieleza Vivian van de Perre, akibainisha kuwa baada ya kupunguzwa kwa wanajeshi kwa 25%, MONUSCO ina na wanajeshi 7,700 pekee nchini DRC.
“Ingawa hii ni kazi mpya, mstari wa kusitisha mapigano uko Kivu Kusini, mkoa ambao tulijiondoa Juni 30, 2024, ikimaanisha kuwa ufuatiliaji wake utahitaji kupelekwa sehemu ya wanajeshie. Kwa hili, rasilimali mpya zinahitajika,” alisema.
Ingawa bajeti ya ziada anayoiomba inapitiwa upya na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, MONUSCO pia inaziomba pande zinazopigana kufungua tena Uwanja wa Ndege wa Kavumu na kuhakikisha harakati huru za walinda amani kama dhamana. Mkutano kati ya Marekani, Rwanda, na DRC ili kukamilisha usitishaji huu wa mapigano unatarajiwa kufanyika mwezi Aprili, huku Kigali ikionekana kuwa tayari zaidi kujadiliana kufuatia vikwazo vilivyowekwa na Marekani.