Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ametangaza kuwa mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran hayana msingi wowote.

Sayyid Abdul Malik Badruddin al Houthi Katibu Mkuu wa Ansarullah ya Yemen amesema: Adui Marekani na Israel zimetenda jinai mbalimbali dhidi ya wananchi Waislamu wa Iran; uvamizi ambao hauwezi kuhalalishwa kwa namna yoyote.

Ameongeza kuwa: Wamarekani na Waisraeli wanafanya njama katika eneo chini ya anwani ” Kuibadilisha Asia Magharibi na Kuanzisha Israel Kubwa”. 

“Njama hii ya Wazayuni imelilenga eneo lote likiwemo Bara Arabu; sasa kuna faida gani  baadhi ya nchi kushirikiana na adui?,” amehoji Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen. 

Sayyid Abdul Malik Badruddin al Houthi amesisitiza kuwa: Hivi sasa ambapo Israel inaushambulia vikali Ukanda wa Gaza bado kuna baadhi ya tawala zinaudhalilisha muqawama na wanamapambano kupitia vyombo vyao vya habari. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *