Chama kikuu cha upinzani nchini Kenya Orange Democratic Movement-ODM kimeendelea kushuhudia mgawanyiko mkubwa baada ya pande mbili zinazopambania uongozi wa chama hicho kilichoanzishwa na Marehemu Raila Odinga, Waziri Mkuu wa zamani kufariki dunia mwezi Oktoba mwaka uliopita, kuandaa mikutano mikuu miwili jijini Nairobi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kundi la Oburu Oginga, ambaye mkutano mkuu wa ODM umemwidhinsisha rasmi kuwa kiongozi wa chama hicho, kumrithi mdogo wake Raila, lilikusanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, kutuma ujumbe kuwa chama hicho bado kipo imara.
Oburu ambaye amesema ameagizwa na mkutano huo mkuu kuanza mazungumzo na chama tawala UDA chake rais William Ruto, ili kuunda muungano mpya kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao, amekanusha madai kuwa amenunuliwa.
“Hatutakuwa kama watu wengine wanaosema ODM imenunuliwa, imenunuliwa na nani?” Amesema Oburu Odinga.
Nalo kundi kundi linaloongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna, aliongoza wafuasi wake kwenye mkutano wao kwenye jumba la Ufungamano. Mkutano wa chama upinzani nchini Kenya ODM
Sifuna na wanasiasa wenzake wameapa kutoondoka kwenye chama hicho, lakini akasisitiza kuwa hawezi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho chini ya Oburu Oginga.
“Nimesema nanataka nirudie, sio lazima Sifuna awe katibu mkuu wa chama cha ODM.” Amesema Sifuna.
Wachambuzi wa siasa wanasema, mgawanyiko huu unaonesha kuwa, chama cha ODM kimeyumba baada ya kifo cha Raila, kuhusu viongozi kutokuwa na msimamo mmoja kuhusu kumuunga mkono rais William Ruto kuwania tena uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.