
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini Tanzania, imesababisha vifo vya zaidi ya watu 20 na kuwaacha wengine bila makaazi, huku hali ikitarajiwa kuwa mbaya.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mbali na kusababisha maafa, Tanzania imeshuhudia pia maporomoko ya udongo siku ya Jumatano katika mkoa wa Mbeya.
Licha ya idadi ya watu waliopoteza maisha kufikia 20, kuna wasiwasi kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka iwapo mvua hiyo itaendelea kunyesha.
Miongoni mwa waliopoteza maisha ni mtoto mchanga mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, aliyesombwa na mafuruko kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Haniu.
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki, zinazoshuhudia mvua kubwa kama ilivyo katika nchi jirani ya Kenya, ambapo mvua iliyosabababisha mafuriko, imewauwa watu zaidi ya 80 na kuwaacha maelfu bila makaazi.
Mamlaka ya hali ya hewa katika nchi hizo mbili zinatoa wito kwa watu wanaoishi kwenye mkondo wa maji kupita, kuhamia katika maeneo yaliyoinuka, kwa sababu ya mvua kubwa inayotarajiwa kuendelea kunyesha hadi mwezi Aprili.