
Janga hilo, lililotokea usiku wa Jumanne, Machi 24, kuamkai Jumatano, Machi 25, limesababisha vifo vya watu wasiopungua tisa na 45 hawajulikani walipo, kulingana na ripoti kutoka Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM). Wahamiaji hao waliondoka kutoka mji wa Obock kaskazini mwa Djibouti, wakitarajia kufika Yemen kupitia Mlango-Bab el-Mandeb, mojawapo ya njia hatari zaidi za uhamiaji duniani, IOM imesema.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu akiwa Nairobi, Gaƫlle Laleix
Zoezi la kutafuta miili zaidi na watu ambao wanaweza kuwa wamenusurika linaendelea nje ya pwani ya Djibouti. Kulingana na walinzi wa pwani wa Djibouti, zaidi ya watu 320 walikuwa katika boti ndogo ya uvuvi karibu na Obock, kaskazini mwa nchi, wakikusudia kufika Yemen kupitia Mlango-Bab el-Mandeb, njia ya maji yenye upana wa kilomita 20 inayotenganisha Pembe ya Afrika na Rasi ya Arabia.
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi, Machi 26, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) liliripoti kwamba watu tisa walifariki katika ajali hiyo na 45 bado hawajulikani walipo, idadi inayoimarisha mtazamo wa shirika hilo kwamba njia hii ya bahari imekuwa mojawapo ya njia hatari zaidi za uhamiaji duniani. Mnamo mwaka 2025, wahamiaji 900 walipoteza maisha wakitumia nji hiyo, lakini hii haijawazuia wale wanaotafuta hifadhi kujaribu kuvuka, kwani idadi yao iliongezeka kwa 20% katika kipindi kama hicho ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Wahamiaji hawa wengi wao kutoka Ethiopia wanakimbia vita vinavyoisambaratisha nchi yao kutafuta fursa nje ya nchi, hasa Saudi Arabia. Lakini mara nyingi, hujikuta wamekwama Yemen, nchi ambayo pia imekumbwa na migogoro, na iko katika hatari ya dhuluma nyingi.
Ingawa wahamiaji waliookolewa wamepelekwa katika kituo cha mapokezi cha IOM huko Obock na uchunguzi umeanzishwa na kitengo cha uchunguzi cha walinzi wa pwani wa Djibouti, shirika hilo linahofia kwamba ajali hii ya botini ya kwanza tu kati ya nyingi mwaka huu. “Msimu wa joto unaanza tu, huku bahari ikiwa na upepo mkali,” anaelezea Tanja Pacifico, Mkuu wa Ujumbe wa IOM nchini Djibouti.