
Chombo cha habari cha Marekani kimetangaza kwamba Iran ndiyo kikwazo kikubwa zaidi kwa nguvu za kijeshi za Marekani tangu baada ya Vita vya Pili vya Dunia.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Mehr, gazeti la Marekani la The New York Times limesema katika ripoti yake kwamba hakuna nchi yoyote, tangu baada ya Vita vya Pili vya Dunia, ambayo imefanikiwa kudhoofisha uwezo wa kijeshi wa Marekani kama Iran.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kutoa changamoto kwa uwezo wa kijeshi na ushawishi wa Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia na dunia katika zama za baada ya Vita vya Pili vya Dunia, na imefanikiwa zaidi katika suala hili kuliko nchi zingine.