Wakati vita vikiingia wiki ya nne mashariki ya Kati, waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen wamesema wameishambulia Israel kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita dhidi ya Iran.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa kundi hilo, umesema limerusha makombora, kulenga ngome muhimu za kijeshi za Israel, ili kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya Israeli nchini Iran na Lebanon.

Houthi wanatishia kuendelea na mashambulizi hayo hadi kile wanachosema, uchozi wa Israeli, utakapokoma.

Awali, Israeli ilitangaza kuwa ilikuwa imefanikiwa, kuzuia kombora lililorushwa na Yemen.

Katika hatua nyingine, Israeli imeendelea kutekeleza mashambulio mazito katika jiji kuu la Iran Tehran na miji mingine, huku nchi jirani ya Saudi Arabia, ikisema imezuia kombora lililokuwa limeelekezwa katika nchi yake.

Aidha, Kuwait nayo imesema, shambulio lililotekelezwa na ndege isiyokuwa na rubani, imesababisha uharibifu mdogo kwenye uwanja wake wa Kimataifa wa ndege, huku Falme ya Kiarabu ikisema imezuia makombora 20 na ndege zisizokuwa na rubani 37 zilizoelekezwa kwenye nchi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *