
Aliyekuwa mwanadiplomasia wa Ubelgiji Etienne Davignon, aliyefunguliwa mashtaka akihusishwa na kifo cha mpigania uhuru na mwanzilishi wa taifa la DRC Patrice Lumumba mwaka 1961, amekata rufaa kupinga kufunguliwa mashtaka.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakili wake Johan Verbist, amesema mwanadiplomasia huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 93, ameamua kukataa rufaa kupinga hatua ya kufunguliwa mashtaka.
Hatua hii inakuja baada ya Mahakama mapema mwezi huu, kumtaka mwanadiplomasia huyo wa zamani kudunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kivita.
Anadaiwa kuhusika na uzuiaji na kusafrishwa kwa Lumumba gerezani, na kunyimwa haki ya kusikilizwa na kuzuiwa kupata haki.
Etienne Davignon ndio mtu pekee ambaye yupo hai kati ya raia 10 wa Ubelgiji, wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya Lumumba, aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Congo baada ya kupata uhuru wake 1960.
Iwapo kesi hii itaendelea, Davignon atakuwa raia wa kwanza wa Ubelgiji kufunguliwa mashtaka miaka 65 baada ya kifo cha Lumumba.
Iwapo Mahakama itafutilia mbali rufaa yake, kesi dhidi yake inatarajiwa kuanza mapema mwezi Januari mwaka 2027.