
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imesema operesheni hiyo lilitekelezwa kwa jina la siri “Ya Rasulullah” na kwa ajili ya kuwaenzi raia na watumishi waliouawa shahidi hivi karibuni walipokuwa wakitumikia sekta ya viwanda vya nchi.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imesema operesheni hiyo lilitekelezwa kwa jina la siri “Ya Rasulullah” na kwa ajili ya kuwaenzi raia na watumishi waliouawa shahidi hivi karibuni walipokuwa wakitumikia sekta ya viwanda vya nchi.
Taarifa hiyo ilisema: “Baadhi ya viwanda vizito vinavyomilikiwa na adui Mmarekani‑Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na maeneo mengine vimepigwa kwa makombora na ndege zisizo na rubani, na sehemu zake zimeharibiwa.”
Taarifa imebaini kuwa: “Wakati wa operesheni hii pana ya makombora na ndege zisizo na rubani, jeshi la anga la adui lilijaribu kulenga vizindua-makombora vyetu kwa kutuma ndege za kivita na droni, lakini ulinzi wa anga wa IRGC uliidungua ndege ya kimkakati isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ‑9 katika anga ya Shiraz, na ndege ya kivita ya Marekani aina ya F‑16 ilipigwa katika kusini mwa mkoa wa Fars na kuangamizwa kabla haijafika kutua katika uwanja wa ndege nchini Saudi Arabia. Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) ilithibitisha katika taarifa kuwa ndege hiyo ilipigwa na kuharibika kabisa.”
Taarifa hiyo ilihitimisha kwa kusema:“Tumekwisha waonya watawala wasio na hekima wa Marekani kwamba tutalipiza kisasi kwa mashambulizi dhidi ya malengo ya viwanda. Shambulizi hili lilikuwa onyo tu; iwapo mashambulizi dhidi ya sekta ya viwanda yatarudiwa, majibu yetu yajayo yatakuwa zaidi ya matarajio yenu.”
Juzi pia Ndege ya kivita aina ya F-18 ya jeshi la kigaidi la Marekani imepigwa na kutunguliwa kwa kombora la Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kusini mwa nchi. Ndege kadhaa za kivita za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zimetunguliwa kwa kutumia makombora ya Iran wakati zikiwa zinatakeleza operesheni za kivita. Siku chache zilizopita, ndege ya kivita ya kimkakati aina ya F‑35 ya Jeshi la Marekani ilipigwa kwa kombora na kuharibiwa vibaya ikiwa katika anga ya kati mwa Iran kwa lengo la kutekeleza mashambulizi. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa ndege hii kulengwa ikiwa vitani.
Aidha Idadi ya ndege zisizo na rubani za maadui zilizotunguliwa na ulinzi wa anga wa Iran hadi sasa inafikia karibu ndege 140.