Baada ya shambulio lililotokea siku ya Jumapili jioni ya Machi 29, serikali ya Jimbo la Plateau imetangaza sheria ya kutotoka nje kwa saa 48 katika kitongoji cha Angwan Rukuba ambapo tkio hilo lilitokea. Hii haikuwazuia wakazi kuandamana, wakidai mamlaka za  kuchukua hatua halisi za kupambana na ukosefu wa usalama.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kufuatia mauaji ya “Jumapili ya matawi,” serikali ya Jimbo la Plateau, katikati mwa Nigeria, ilitangaza amri ya kutotoka nje ya saa 48 katika eneo ambalo tukio hilo lilitokea Jumatatu, Machi 30.

Jioni ya siku ya Jumapili, yapata saa 2:30 usiku, watu wasiojulikana, wenye silaha nzito walifyatua risasi katika baa nje kidogo ya Jos, mji mkuu wa jimbo, na kuua watu kadhaa. Angalau watu 30 waliuawa katika shambulio la baa katika kitongoji cha Angwan Rukuba, huku watu wengine watatu baadaye wakipoteza maisha katika ghasia hiyo wakati umati ukijaribu kuwafuata na kuwaadhibu washambuliaji.

Eneo linalokumbwa na vurugu za kijamii mara kwa mara

Wakati mvutano ukiendelea kuwa mkubwa huko Jos, chuo kikuu cha eneo hilo na shule kadhaa karibu na eneo la tukio la mauaji zilitangaza kusitisha masomo siku ya Jumatatu. Wakazi wengi waliandamana mitaani kudai mamlaka kuchukua hatua madhubuti za kupambana na ukosefu wa usalama, hata wakipuuza sheria ya kutotoka nje iliyowekwa na mamlaka.

Mnamo Machi 14, katika eneo hilo la Plateau, ambalo mara kwa mara hukabiliwa na vurugu za kijamii, watu wenye silaha waliwaua watu 20 na kuiba mifugo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *