Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ametoa shukrani zake kwa wanazuoni wa Kisunni katika Mkoa wa Kurdistan nchini Iran kufuatia ujumbe wao wa pole na mshikamano baada ya kuuawa kishahidi kwa aliyekuwa Kiongozi, Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Katika ujumbe uliotumwa kwa wanazuoni wa Ahlul Sunna wa Kurdistan siku ya Jumanne, Kiongozi Muadhamu amewashukuru kwa salamu zao za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran, akionyesha pia shukrani kwa hisia zao njema walizoonesha kwake.

Sehemu ya ujumbe huo imesomeka hivi:  “Wanazuoni waheshimiwa wa Mkoa wa Kurdistan; natoa shukrani kwa kuonesha kwenu pole na rambirambi juu ya kuuawa kishahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran, pia nawapongeza na kuwashukuru kwa wema na upendo mlionionesha mimi.”.

Ayatullah Khamenei pia amepongeza msimamo “ulio wazi na thabiti” wa wanazuoni wakuu wa kidini wa Iraq pamoja na wananchi wa nchi hiyo kuhusu vita vya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ayatullah Mojtaba Khamenei ameuthamini msimamo wa wazi wa mamlaka ya kidini ya Iraq na taifa hilo kuhusu mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Aidha aliwaombea dua ya mafanikio endelevu, akimwomba Mwenyezi Mungu awajaalie ustawi na kuwapa nguvu katika kuendelea kuutumikia Uislamu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei aliuawa shahidi  katika shambulio la kigaidi la Marekani na Israel lililolenga ofisi yake tarehe 28 Februari, sawa na tarehe 10 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, siku ya kwanza ya vita vinavyoendelea dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Wanafamilia kadhaa pia waliuawa kishahidi katika tukio hilo, akiwemo binti yake, mkwe wake wa kiume, mkwe wake wa kike pamoja na mjukuu wake.

Vikosi vya jeshi la Iran vinaendelea kujibu  uchokozi huo kwa kuvurumisha mfululizo wa makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya ngome za kijeshi na kiuchumi utawala wa  Kizayuni waIsrael pamoja na vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyonchi za eneo la Asia Magharibi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *