Mwaka huu, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, hatua muhimu inayodhihirisha safari nde­fu ya nusu karne kujenga na kusi­mamia ubora wa bidhaa na huduma nchini.

Katika kipindi hiki cha nusu karne, TBS imekuwa mhimili mkubwa wa kulinda afya ya walaji, kukuza ushin­dani wa bidhaa za ndani na kuhaki­kisha Tanzania inashiriki kikamilifu katika biashara ya kimataifa.

TBS ilianzishwa mwaka 1975 na kuanza kutekeleza majukumu yake rasmi mwaka 1976 chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kama seh­emu ya jitihada za Serikali katika kuimarisha miundombinu ya sekta za viwanda na biashara ili kukuza uchumi wa Taifa na linatekeleza majukumu yak echini ya sheria ya viwango sura 130.

Hata hivyo, kadri uchumi wa Tan­zania ulivyokua na mahitaji ya soko kubadilika, TBS ilipanua wigo wake na kuwa taasisi yenye ushawishi mkubwa katika sekta ya viwanda, biashara na afya ya jamii.

Ukuaji wa TBS ndani ya miaka 50

Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi anasema katika kipindi cha miaka 50, TBS imekua kwa kasi kubwa na kupata mafanikio makubwa hususani katika utekeleza­ji wa majukumu yake. Mafanikio hayo yameendelea kutimiza azma ya Serikali katika sekta ya biashara hususani kuwezesha biashara iki­wa ni pamoja na kuwasaidia wazal­ishaji kufikia masoko la kikanda na kimataifa.

Dkt. Katunzi anasema katika kipin­di hicho pia shirika hilo limeshuhudia ukuaji mkubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo miundombinu ambapo wakati linaanzishwa lilikua na ofisi ndogo iliyokuwa imejeng­wa kwa mabati lakini hivi sasa lina jengo kubwa ambalo lina miundom­binu za kisasa, uwe­po wa maabara za kisasa pamoja na ujenzi wa maabara mpya katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Mwanza.

“Wakati shirika linaanzishwa kuli­kuwa na ofisi moja pekee iliyoku­wepo Dar es Salaam lakini hivi sasa tuna ofisi kwenye mipaka, bandarini, viwanja vya ndege pamoja na ofisi za kanda tisa (Kanda ya Maghari­bi, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa Mashariki, Kanda ya Ziwa Magharibi, Kanda ya Dar es Salaam na Kanda ya Kusini),” anasema Dk Katunzi.

Kuongeza idadi ya wafanyakazi ambao Dkt. Katunzi anasema wakati TBS inaanzishwa ilikuwa na wafa­nyakazi 30 pekee lakini hivi sasa ina wafanyakazi zaidi ya 800. Shirika pia limekuwa kimbilio la wafanya­biashara na wajasiriamali katika kuhakikisha bidhaa zao zinafika kati­ka masoko ya kimataifa.

“Hivi sasa TBS imekuwa kimbilio la wafanyabiashara na wajasiriamali kuelekea masoko ya kimataifa. Hili ni jambo kubwa kwani wakati linaan­zishwa watu walikuwa hawalielewi lakini hivi sasa limekuwa kimbilio lao,” anasema Dkt Katunzi.

Dkt. Katunzi anasema pia shirika hilo limeimarisha ukaguzi bidhaa kutoka nje Pre-Verification of Con­formity (PVOC) ili kutatua chan­gamoto ya bidhaa hafifu zinazoingia nchini.

“Mfumo huu unahakikisha bidhaa zote zinazoingizwa nchini zin­akidhi viwango vilivyowekwa kabla hazijaingia sokoni. Hii imechangia kupunguza bidhaa hafifu sokoni,” anasema Dkt. Katunzi.

Uandaaji wa viwango

Moja ya majukumu makuu ya TBS ni kuandaa viwango vinavyotumika kudhibiti ubora wa bidhaa na hudu­ma. Hadi sasa, maelfu ya viwango vimeandaliwa katika sekta mbalim­bali kama vile chakula, ujenzi, kemi­kali, na bidhaa za viwandani.

“Shirika lina kamati za kitaalamu za uandaaji viwango 117 katika sek­ta za chakula, kemikali, uhandisi mitambo, uhandisi umeme, uhandisi ujenzi, nguo na ngozi, madini na mitambo ya uchim­baji madini, mazingira na sekta nyingine mtambuka,” anasema Dkt. Katunzi.

Dkt. Katunzi anasema katika mchakato wa kuandaa viwango, kamati hizo zinashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo vyuo vikuu, taasisi za utafiti, wafanyabiashara, wazalishaji, vyama vya walaji, bodi za wataalamu,

“Kwa kipindi cha miaka 50 shirika limefanikiwa kuandaa viwango zaidi ya 4000 vya sekta mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji ya soko ambavyo vinasaidia wafanyabiashara, waja­siriamali na watoa huduma kuzali­sha bidhaa bora zinazopata masoko nje ya nchi,” anasema Dkt. Katunzi.

Umahiri na vifaa bora vya Maabara

Katika kuhakikisha ubora wa huduma zake, TBS imewekeza kwa kiasi kikubwa katika maabara za kisasa. Maabara hizi zina vifaa vya hali ya juu vinavyowezesha kufanya vipimo sahihi na vya kuaminika.

“TBS ina jumla ya maabara 12 na zote zina ithibati za umahiri ambapo maabara hizi zimahakikiwa na kupa­tiwa vyeti vya ithibati ya umahiri wa kimataifa. Hatua hii inamaanisha kuwa majibu ya sampuli kutoka kati­ka maabara hizo yanaaminika kokote duniani na hivyo kurahisisha biasha­ra ndani na nje ya mipaka ya Tanzania,” anasema Dkt. Katunzi.

Anasema maabara zote za TBS zina mashine na vifaa vya kisasa hivyo kuwezesha kupata majibu kwa wakati na sahihi. Aidha katika kuunga mkono ajenda ya Serikali ya matumizi ya nishati safi ya kupikia, TBS ina maabara maalumu ya kupi­ma viwavyo vya vifaa vinavyotumia nishati safi kutoka ndani na nje ya nchi (energy efficiency laboratory).

Uwekezaji katika mifumo ya TEHA­MA

Katika zama za kidijitali, TBS haijabaki nyuma. Shirika limeweke­za katika mifumo ya TEHAMA ili kuboresha utoaji wa huduma, kuongeza uwazi na kurahisisha mawasiliano na wadau.

Dkt. Katunzi anasema wali shiri­ka hilo lilikuwa linafanya shughuli zake kwenye makaratasi lakini hivi sasa kila huduma inapatikana katika mifumo jambo lililoongeza ufanisi wa utoaji huduma hivyo kulifanya shirika kuwa la kisasa na kuaminika zaidi.

“Kwa sasa shirika linatumia mifu­mo ya TEHAMA katika utoaji wa huduma zake mbalimbali kama vile leseni ya ubora, ukaguzi wa she­hena zinazotoka nje na usajili wa bidhaa za chakula na vipodozi. Mifu­mo hiyo ni OAS na i-SQMT. Aidha shirika limeboresha huduma zake kwa wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa kutoka nchini kwa kuungan­isha mfumo wake wa OAS na mfumo wa dirisha moja la huduma (TeSWS) ambapo mfanyabiashara anatuma maombi na kupata huduma za taasisi zote na kibali katika mfumo mmoja,” anasema Dkt. Katunzi.

Tuzo za umahiri na kutambulika kimataifa

Kwa juhudi zake katika kusimamia ubora, TBS inatambulika kimatai­fa na kushinda tuzo mbalimbali za umahiri. Mwaka 2023 TBS ilishinda tuzo ya mdhibiti bora barani Afrika na taasisi bora ya udhibiti Tanzania 2025, vilevile TBS imekuwa taasisi ya kwanza katika ukanda wa SADC kupata ithibati ya mifumo ya udhibiti ubora wa bidhaa katika wigo mpana ndani ya muda mfupi.

Vilevile TBS ina idhibati ya uma­hiri wa kimataifa katika mfumo wa Ukaguzi (ISO/IEC 17020. Mwaka 2025 TBS ilifanikiwa kupata ithibati ya umahiri wa mfumo wa usimam­izi wa chakula katika kiwango cha kimataifa toleo jipya (ISO 22003: 2022). Pia shirika hilo kupitia wataa­lamu wake liliweza kutoa mshindi wa ISO Next Generation Award mwaka 2023.

Maadhimisho ya miaka 50

Dkt. Katunzi anasema kuwa katika kusherehekea miaka 50, TBS imean­daa matukio mbalimbali ambapo Mei 23, 2026 watafanya mbio za hisani (Viwango Marathon) zitakazofan­yika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam, Juni 5, 2026 wata­fanya jukwaa la kibiashara (Viwan­go Business Forum) litakalofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Pia kutakuwa na zoezi la kurudisha kwa jamii (CSR) kabla ya hafla ya kilele cha maadhimisho hayo itakayofanyika Juni 19, 2026 jijini Dodoma.

Maadhisho ya miaka 50

Dk Katunzi anasema kuwa katika kusherehekea miaka 50, TBS imean­daa matukio mbalimbali ambapo Mei 23, 2026 watafanya mbio za hisani (Viwango Marathon) zitakazofan­yika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam, Juni 5, 2026 wata­fanya jukwaa la kibiashara (Viwan­go Business Forum) litakalofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Pia kutakuwa na zoezi la kurudisha kwa jamii (CSR) kabla ya hafla ya kilele cha maadhimisho hayo itakayofanyika Juni 19, 2026 jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *