#HABARI: Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan, ametoa wito wa kuboresha miundombinu ya michezo katika Shule ya Msingi Kitunga iliyopo wilayani Muleba ili kuongeza hamasa ya michezo kwa jamii.

Akizungumza kwenye fainali za Ramadhan Coffee Cup, Faris amesisitiza haja ya kubadilisha milingoti ya mbao na kuweka ya chuma katika uwanja wa Kitunga Arena ili uwe wa kisasa zaidi.

Katika kufanikisha azma hiyo, Faris amefanikisha upatikanaji wa ahadi za kifedha kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo huku yeye mwenyewe akichangia fedha za kununulia nyavu za kisasa na vifaa vya uratibu.

Juhudi hizi zinalenga kuinua kiwango cha soka wilayani Muleba na kuhakikisha vijana wanapata mazingira bora ya kukuza vipaji vyao kupitia mashindano kama hayo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *