Wakati huu Wakristo nchini Uganda wakijiandaa kuadhimisha Pasaka, msimu ambao kwa kawaida huambatana na watu kusafiri, familia kukutana na sherehe, wengi safari hii wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha kutokana na kupanda kwa bei za mafuta ambazo zinaongezeka kwa kasi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ongezeko la bei linalosababishwa na migogoro kwenye eneo la Mashariki ya Kati, linaonekana kuanzia mijini kama Kampala hadi vijijini ambapo gharama za usafiri huathiri moja kwa moja maisha ya watu.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, athari haishuhudiwi Uganda peke yake, nchi kama Kenya na Tanzania, ambazo hutumika kama njia muhimu za usafirishaji wa mafuta, pia zinakabiliwa na kupanda kwa gharama za uagizaji na usafirishaji.

Kwa Uchumi wa nchi zisizo na Bahari ikiwa ni pamoja na Rwanda, Burundi, DRC na Sudan Kusini, ziko katika hatari kubwa, kwakuwa usumbufu wowote katika korido hizi kutasababisha bei ya mafuta kupanda na kuongeza gharama za usafiri.

Wachambuzi wa nishati wanaonya kuwa, ikiwa mgogoro wa Iran utaendelea, eneo hili linaweza kukabiliwa na vikwazo vikubwa vya usambazaji na kupanda kwa bei zaidi na kutokea kwa mfumuko wa bei ambao tayari baadhi ya kaya zimanza kuhisi maumivu.

Mlango Bahari wa Hormuz ambao unadhibitiwa na Iran kwa sasa, ndio njia kuu ya ugavi wa mafuta duniani, ambapo zaidi ya asilimia 20 ya mafuta ya dunia hupitia hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *