Mkuu wa NATO, Mark Rutte, atakutana na Donald Trump huko Washington siku ya Jumatano, siku moja baada ya rais wa Marekani kutangaza kusitisha mapigano kwa wiki mbili na Iran. Wakati rais wa Marekani anatishia kujiondoa kutoka Muungano wa Atlantiki, amekuwa akimsifu Katibu Mkuu wa shirika hilo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mark Rutte pia atakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio na Waziri wa Ulinzi, Pete Hegseth. Kulingana na afisa mmoja wa NATO, ziara hii nchini Marekani ilipangwa “kwa muda mrefu.”

Mbali na kuimarisha ushirikiano wa nchi za ng’ambo ya Atlantiki katika sekta ya ulinzi, maafisa hao wawili wanatarajiwa “kujadili mienendo ya sasa ya usalama, katika muktadha wa vita vya Iran na Urusi dhidi ya Ukraine,” afisa huyo ameongeza.

Makubaliano ya kusitisha mapigano na Iran ni “ushindi” kwa Marekani, kulingana na Ikulu ya White House

Wakati mazungumzo kati ya pande hizo mbili yaliyopangwa kuanza Ijumaa, Aprili 10, nchini Pakistan, makubaliano ya kusitisha mapigano na Iran ni “ushindi” kwa Marekani, anasema msemaji wa Ikulu ya White House. 

“Huu ni ushindi kwa Marekani, uliowezeshwa na Rais Trump na vikosi vyetu vya kijeshi,” Karoline Leavitt ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *