Wakati wa ziara yake katika nchi ya Simba wa Teranga, ambao taji lao la Kombe la Mataifa ya Afrika lilifutwa na bodi ya rufaa ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) mnamo Machi 17, kiongozi wa CAF, siku ya Jumatano, Aprili 8, alitaka kutuliza sintofahamu iliyojitokeza. 

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff

Akielezea wasiwasi wake kuhusu hatima ya mashabiki 18 wa timu ya taifa ya soka ya Senegal ambao bado wanazuiliwa nchini Morocco kufuatia vurugu zilizokumba mchezo wa fainali wa AFCON kati ya nchi mwenyeji, Morocco, na Senegal, mnamo Januari 18, Motsepe pia alisema yuko tayari kwa aina yoyote ya uchunguzi kuhusu ufisadi unaoshukiwa ndani ya taasisi yake.

Karibu mwezi mmoja baada ya uamuzi wa kuivua Senegal taji lao la Kombe la Mataifa ya Afrika na kulikabidhi kwa Morocco, Patrice Motsepe, Mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), alifanya ziara Jumatano, Aprili 8, nchini Senegal, ambapo alikutana na viongozi wa Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) na Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye. Lengo la ziara hii ya kidiplomasia: kuirekebisha CAF, ambayo sasa inakabiliwa na ukosoaji mkubwa nchini Senegal.

Wakati wa ziara yake, Patrice Motsepe kwanza alitaka kuwatuliza raia wa Senegal, akisema kwamba masomo yamepatikana baada ya vurugu zilizoukumba mchezo wa fainali wa AFCON mnamo Januari 18 kati ya Morocco na Senegal. “Mara tu baada ya fainali huko Morocco, tulimwita mwenyekiti wa kamati ya waamuzi.” “Maswali mengi yaliulizwa kwake,” alielezea awali. “Lakini kwa kuwa kesi hiyo iko mbele ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), hatuwezi kuingia kwa undani zaidi, ili tusije kushtumiwa kushawishi kesi inayochunguzwa,” aliongeza.

“Sina shaka kwamba tutatoka katika mgogoro huu tukiwa tumeungana na kuwa na nguvu zaidi. Kilichotokea Morocco kitakuwa somo muhimu.”

Rais wa CAF kisha kwa uangalifu alishughulikia suala lingine linaloikera Dakar: hatima ya mashabiki 18 wa timu ya taifa ya soka ya Senegal ambao bado wanazuiliwa huko Rabat, hali ambayo inaharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili. “Hili ni jambo linalotutia wasiwasi, lakini kutokana na unyeti wake, haya ni majadiliano ambayo hatutaki kuyaweka hadharani.” “Hata hivyo, katika ngazi ya kidiplomasia, viongozi wamearifiwa,” alisema.

Kuhusu nia ya Dakar ya kufungua uchunguzi huru kuhusu tuhuma za ufisadi ndani ya CAF, Patrice Mostepe alisema yuko tayari: “Ninahimiza aina yoyote ya uchunguzi kuhusu ufisadi, iwe unatoka kwa serikali au mtu binafsi. Ninahimiza na kuunga mkono mpango wa aina hii kwa sababu tunataka kufahamu visa vyovyote vya ufisadi ndani ya CAF,” alibainisha.

Baada ya ziara yake fupi nchini Senegal, Patrice Mostepe alisafiri hadi Morocco siku ya Jumatano jioni, ambapo anatarajiwa kukutana na viongozi wa Shirikisho la Soka la Morocco (FMF) na serikali leo Alhamisi, Aprili 9.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *