
Jeshi la Nigeria limetangaza Jumapili, Aprili 5, kwamba liliwaokoa waumini 31 waliotekwa nyara wakati wa sherehe za Pasaka katika kijiji cha Ariko, katika Jimbo la Kaduna, kaskazini magharibi mwa Nigeria. Watu watano waliuawa katika shambulio hilo, licha ya uwepo mkubwa wa vikosi vya usalama karibu na makanisa wakati wa sikukuu hiyo. Hata hivyo, wanakijiji na viongozi wa kidini wanapinga kauli ya jeshi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika taarifa yake kwenye mtandao wa kijamii wa X, jeshi linaelezea operesheni hiyo kama ushindi. Kulingana na jeshi, wanajeshi “waliwafuata” “magaidi” waliohusika na shambulio hilo kutokana na “nguvu na silaha” waliokuwa nazo, na waliweza kuwalazimisha washambuliaji kuwaacha mateka walipokuwa wakikimbia. Lakini toleo hili rasmi haliendani na masimulizi ya mashahidi kutoka eneo hilo.
Kauli “za Uongo na zinazopotosha”
Siku ya Jumatatu, Aprili 7, baada ya kuzungumza na wakazi, Mchungaji John Hayab wa Chama cha Wakristo cha Nigeria huko Kaduna alikanusha kauli ya jeshi kwenye vyombo vya habari. Chama kwa ajili ya Maendeleo ya Kuturmi pia kilifutilia mbali toleo la jeshi: “Wale wote waliotekwa nyara bado wanashikiliwa mateka.” Katika taarifa yake, cama hicho kilishutumu kauli hizo kama “za uwongo na za kupotosha.”
“Mkanganyiko”
Wakati huo huo Joseph Ariko, mmoja wa viongozi wa jamii huko Ariko, anaelezea nadharia ya “mkanganyiko” kwa upande wa jeshi. “Dada yangu mkubwa, binamu yangu, na watoto wake walikuwa kanisani na walitekwa nyara. Kama wangeokolewa, ningejua.” Siku ya Jumanne jioni, Aprili 7, bado alikuwa akihesabu watu 35 waliotoweka kutoka kijijini baada ya shambulio.