
Hatua ya Israeli, kuendelea kutekeleza mashambulio mazito nchini Lebanon, kunazua maswali iwapo mkataba wa kusitisha vita kwa wiki mbili kati ya Marekani na Iran, utaendelea kutekelezwa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Israeli imeendelea kushambulia Lebanon, wakiwalenga wapigani wa Hezbollah, katika mashambulizi ambayo nchi hiyo na Marekani, zinasema, Lebanon haipo kwenye mkataba wa kusitisha vita.
Mashambulizi ya Israel yameendelea kutikisa Lebanon, ambayo leo imekuwa ni siku ya maombolezo ya kitaifa baada ya kuuawa kwa watu 200 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 1000 kwa siku moja siku ya Jumatano.
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema mashambulizi ya Israeli nchini Lebanon yanakiuka mkataba wa kusitsha vita, na huenda mazungumzo yatakayoanza siku ya Ijumaa, yakakosa maana akiongeza kuwa Iran haitowaacha raia wa Lebanon.
Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema nchi yake itaendelea kuishambulia Lebanon, licha ya mkataba kati ya Iran na Marekani, huku jeshi la nchi yake likiwataka wakaazi katika baadhi ya mitaa ya jiji kuu Beirut kuondoka.
Naye rais wa Marekani wa Marekani amesema, wanajeshi wa nchi yake, wataendelea kusalia katika eneo la Mashariki ya Kati, hadi pale Iran itakapoheshimu na kutekeleza kwa kikamilifu mkataba wa kusitisha vita.