
Mazungumzo ya awali yasiyo ya moja kwa moja, yatakayosimamiwa na mamlaka ya Pakistan, yamepangwa kuanza kesho kati ya Iran na Marekani, ambazo zina siku kumi na tano kufikia makubaliano ya kusitisha vita.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa saa 48 zilizopita, suala la Lebanon limekuwa mstari mwekundu kufuatia mashambulizi mabaya ya anga ya Israel huko Beirut, licha ya usitishaji mapigano.
Pakistan itatoa visa kwa wajumbe wote Watakaowasili Islamabad
Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Ishaq Dar ametangaza kwamba wajumbe wote, wakiwemo waandishi wa habari wataosafiri kwenda Islamabad kwa mazungumzo kuhusu usitishaji mapigano kati ya Iran na Marekani watapewa visa watakapowasili Pakistan.
“Pakistan inawakaribisha wajumbe wote, wakiwemo waandishi wa habari kutoka nchi, wanaosafiri kwa ajili ya mazungumzo ya Islamabad 2026,” Ishaq Dar amesema katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X. “Kwa lengo hili, mashirika yote ya ndege yanaombwa kuwaruhusu watu hawa kupanda ndege bila visa. Mamlaka ya uhamiaji ya Pakistan itawapa visa watakapowasili.”