Klabu ya Fountain Gate FC imethibitisha rasmi kumteua Fred Felix Minziro “Majeshi” kuwa Kocha Mkuu mpya, akichukua nafasi ya Mohamed Laizer aliyesimamishwa kazi kutokana na matokeo yasiyoridhisha ya timu.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, Minziro ataiongoza benchi la ufundi kwa kushirikiana na makocha wasaidizi Mathias Wandiba na Abubakari Ally Francis, ambaye ataendelea na majukumu yake ndani ya kikosi.

Uamuzi huo umefanyika wakati Fountain Gate FC ikishika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC (NBCPL), ikiwa imecheza mechi 17 na kujikusanyia alama 16. Uongozi wa klabu una matumaini kuwa mabadiliko hayo yataleta msukumo mpya na kuboresha matokeo katika michezo ijayo.

#kilichoborakabisa

(Feed generated with FetchRSS)

One thought on “Klabu ya Fountain Gate FC imethibitisha rasmi kumteua Fred Felix Minziro “Majeshi” kuwa Kocha Mkuu mpya, akichukua nafasi ya Moh…”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *