
Wadjibouti wamepiga kura jana, Ijumaa, kumchagua rais wao. Rais aliye madarakani Ismaïl Omar Guelleh amechaguliwa tena kwa asilimia 97.81 ya kura, kulingana na matokeo rasmi yaliyotangazwa leo Jumamosi. Hakuna matukio mabaya hususan vurugu zilizoripotiwa kwa siku ya jana Ijumaa, Aprili 10.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wapiga kura 256,000 waliitwa kuchagua kati ya wagombea wawili: Ismaïl Omar Guelleh, 78, ambaye tayari amehudumu kwa miaka 27 kama rais wa Djibouti, akigombea tena kama mgombea wa Muungano wa Wengi wa kami ya rais (UMP), na Mohamed Farah Samatar, mpinzani pekee na kiongozi wa chama kidogo, cha CDU. Mgombe huyu alipata asilimia 2.19 ya kura, kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani, ambazo zitathibitishwa na Baraza la Katiba.
Saa 1:00 usiku kwa saa za ndani, wakati vituo vya kupigia kura vilipofungwa siku ya Ijumaa, mamlaka zilielezea kuridhika kwao na jinsi siku ya uchaguzi ilivyokuwa. “Zoezi la upigaji kura lilifanyika kwa utulivu na amani na hakukuwa na matukio yoyote mabaya…,” Bahnan Ali Maidal, mwenyekiti wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI), aliwaambia waandishi wa habari.
Kuhusu wagombea, Ismaïl Omar Guelleh, rais aliye madarakani, ambaye alipiga kura mapema asubuhi katika mji mkuu, Djibouti, alionyesha “imani yake katika matokeo ya uchaguzi huu,” ambapo anatarajia “uungwaji mkono mkubwa kwa ugombea wake.”
Alikuwa akigombea dhidi ya Mohamed Farah Samatar, mwanachama wa zamani wa chama cha rais na asiyejulikana sana kwa umma, kiongozi wa chama kidogo cha kisiasa kisicho na maafisa waliochaguliwa katika ngazi ya mitaa au kitaifa.
Vyama vikuu vya upinzani vilisusia uchaguzi. Hasa, ARD, MRD, na washirika wao waliona mchakato wa uchaguzi kuwa wa udanganyifu, usio na uwazi, na unaodhibitiwa kikamilifu na vyombo vya dola. Kundi hili hilo la upinzani limetoa wito wa “mabadiliko ya kidemokrasia yatakayojadiliwa, chini ya usimamizi wa jumuiya ya kimataifa.”