MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afri ka (AFCON 2027) inatarajiwa kuanza Juni 19 na kumalizika Julai 18, mwakani.
Shirikisho la Soka Africa (CAF) limethibitisha hivi karibuni, ambapo michuano hiyo itaandaliwa kwa ushikiano wa nchi tatu za Afrika Mashariki; Tanzania, Kenya na Uganda.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa Afcon kuandaliwa kwa pamoja na mataifa matatu, jambo linalota rajiwa kuongeza ushindani na ushirikiano wa kikanda.
Mashindano hayo yanataraji wa kuwa ya kihistoria, yakishirik isha jumla ya timu 28 badala ya 24 kama ilivyokuwa Morocco msimu uliopita wa michuano hiyo.
Aidha, Afcon 2027 itakuwa ya mwisho kufanyika kwa kipindi cha kila baada ya miaka miwili kwani kuanzia 2028 itahamia rasmi kwenye mfumo mpya wa kila baada ya miaka minne.
Tukio hilo pia linaashiria kure jea kwa michuano hiyo katika ukanda wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashari ki na Kati (CECAFA), baada ya takribani miongo kadhaa tangu ilipofanyika mara ya mwisho mwaka 1976 nchini Ethiopia.
Hivi karibuni imeshuhudiwa maandalizi yakiendelea katika nchi husika kuhakikisha miun dombinu na viwanja vinakidhi viwango vya kimataifa.
