
Mazungumzo kati ya Marekani, Iran na Pakistan yameanza siku ya Jumamosi jijini Islamabad, yakiwa ni mazungumzo ya kwanza ya hali ya juu kuwahi kufanyika kati ya Washington and Tehran tangu mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1976.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Makamu wa rais J D Vance anaongoza ujumbe wa Marekani na kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo, alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif.
Mazungumzo hayo sio ya ana kwa ana kati ya Iran na Marekani , chini ya upatinishi wa Pakistan.
Upande wa Iran, unaongozwa na Spika wa bunge Mohammad Bagher Ghalibaf na Waziri wa Mambo ya nje Abbas Araghchi, na yanalenga kutafuta suluhu ya kudumu kuhusu vita ambavyo vimekuwa vikiendelea.
Pakistan kwa upande wake, inasema inajitahidi kuhakikisha kuwa mazungumzo hayo ni ya moja kwa moja ili kumaliza vita hivyo vya wiki sita.
Rais Donald Trump kwenye ukursa wake wa kijamii wa Thruth, amesema Iran inapoteza vibaya kwenye mzozo huo, huku Iran ikionya kuwa mazungumzo hayo yanaweza kufutwa iwapi masharti yao hayatekelezwa.