Nchini Senegal, mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 24 alihukumiwa siku ya  Ijumaa, Aprili 10, kifungo cha miaka sita jela na kutozwa faini ya faranga za CFA milioni mbili na mahakama huko Pikine-Guédiawaye, kitongoji cha Dakar. Hii ni hukumu ya kwanza ya sheria iliyotangazwa mwezi uliopita ambayo huongeza maradufu adhabu za juu zaidi, sasa hadi miaka kumi. Tangu mwezi Februari, watu wapatao sitini wamekamatwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Dakar, Juliette Dubois

Mfanyakazi huyu mwenye umri wa miaka 24 ambaye alikamatwa akitekeleza kitendo ushoga huko Pikine,  anakuwa mtu wa kwanza kuhukumiwa chini ya sheria mpya.

Sheria hiyo iliyopitishwa na wabunge 135 kati ya 165 mnamo Machi 11, na kutiwa saini mwishoni mwa mwezi Machi na rais Diomaye Faye—licha ya wito kutoka kwa mashirika ya kimataifa ya Haki za Binadamu ya Amnesty International na Human Rights Watch (HRW) wa kuibatilisha—inaongeza maradufu adhabu, sasa kutoka miaka mitano hadi kumi jela, na pia inaharamisha “kukuza” ushoga wowote.

Hukumu hii inakuja katikati ya hali ya ukandamizaji mkali. Tangu mwanzoni mwa mwezi Februari, watu wamekuwa wakikamatwa karibu kila siku—karibu watu zaidi ya sitini walikamatwa kulingana na hesabu ya hivi karibuni—mara nyingi hukamatwa kulingana na shutuma au baada ya upekuzi wa simu. Majina ya waliokamatwa yanawekwa hadharani, na kuwaweka watuhumiwa katika hali ya hatari. Baadhi pia wanashutumiwa kwa kusambaza VVU kimakusudi.

Kesi zingine tayari ziko mahakamani, huku washukiwa kadhaa walizuiliwa katika siku za hivi karibuni. Kutokana na hali hii, idadi inayoongezeka ya wapenzi wa jinsia moja wanatafuta kuondoka Senegal. Shirika la STOP Homophobie kutoka Ufanrasa limepokea maombi karibu 200 ya msaada katika wiki chache tu. Idadi hii inaongezeka kila mara, na mkurugenzi wake anasema hawawezi tena kukabiliana nayo. Ufaransa imeiainisha Senegal kama nchi yenye hatari kubwa kwa watu wa LGBT+ tangu mwaka 2021, lakini taratibu za kutoa hifadhi za ukimbizi zinaendelea kuwa ndefu na zisizo na uhakika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *