
Watu zaidi ya 30 wamepoteza maisha baada ya boti waliyokuwa wanasafiria kuzama, kwenye Ziwa Tanganyika, karibu na mji wa Kalemie, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mtumbwi huo wenye uwezo wa kuchukua takriban watu 50, uliondoka katika mji wa Katibili, kilomita 30 kusini mwa mji wa Kalemie. Mwendo wa saa 10 asubuhi Jumatatu, boti hiyo ilizama ziwani Tanganyika karibu na kijiji cha Kibanga, takriban kilomita kumi kutoka Kalemie.
Mapema, wanakijiji walipanga msako wa kuwatafuta waathiriwa na walionusurika. Idadi ya vifo kwa muda ni kubwa. Watu 30 walipoteza maisha, alihakikisha mea wa Muji Kalemie, David Mukeba. Baazi yao kuna wanawake na watoto. Abiria 5 walinusurika.
Hata hivyo, idadi kamili ya abiria kwa sasa haijulikani. Boti hiyo ilisafiri bila kuwa na taarifa ya abiria. Chanzo kilicho karibu na polisi wa baharini huko Kalemie kinakemea kukosekana kwa uangalizi wowote wa bandari ndogo ambako meli hiyo ilikuwa na makao yake. Kwa sasa, kamishna wa polisi wa baharini huko Kalemie, tulie mpigia simu, hakujibu.