MBEYA CITY: “…tunataka pointi tatu muhimu….”
Kikosi cha Mbeya City tayari kipo Dar es Salaam, kuwakabili Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Aprili 16, 2026 kwenye Dimba la KMC Complex.
Kuelekea mchezo huo, Afisa Habari wa Mbeya City, Gwamaka Mwankota, anasema maandalizi yote yamekamilika huku akiwajibu wanaodai kuwa timu yao imetumwa, akisema “…sisi siyo bundi wala siyo paka”
Nao baadhi ya wachezaji wamesema wanachokitaka ni pointi tatu, huku wakikumbushia yaliyojiri kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliomalizika kwa suluhu mkoani Mbeya.
Soud Dondola anasema “…Yanga wanapokutana na Mbeya City, ni Dabi”
Je, wewe unasemaje?
#NBCPremierLeague #MbeyaCity
(Feed generated with FetchRSS)