
Iran imetishia siku ya Jumatano, Aprili 15,kuzuia Bahari Nyekundu ikiwa Marekani itaendelea kuzuia bandari zake, ikisema kwamba inaweza kusababisha ukiukaji wa usitishaji mapigano wa sasa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Iran imesema siku ya Jumatano kwamba mazungumzo na Marekani yalikuwa yakiendelea, kupitia Pakistan, baada ya majadiliano yao huko Islamabad kuvunjika mwishoi mwa wiki iliyopita.
Marekani, kwa upande wake, imekana kukubali kuongezwa muda wa kusitisha mapigano na Iran.
Hata hivo duru za kuaminika zinabaini kwamba Wapatanishi wamekaribia Jumatano kuongeza muda wa kusitisha mapigano kati ya Marekani na Iran na kuanzisha tena mazungumzo ili kuokoa makubaliano dhaifu ya wiki mbili.*
Afisa mkuu wa Marekani aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina kwa sababu hakuruhusiwa kujadili hadharani mazungumzo hayo nyeti, amesema Marekani haijakubali rasmi kuongeza muda wa kusitisha mapigano na kwamba mazungumzo na Iran yanaendelea.
Kamanda wa kamandi ya pamoja ya jeshi la Iran, Ali Abdollahi, ameonya kwamba Iran itazuia kabisa mauzo ya nje na bidhaa zinazoingizwa katika eneo la Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Oman na Bahari ya Shamu ikiwa jeshi la Marekani halitaondoa kizuizi chake kwenye bandari za Iran.