AZAM FC vs JKT TANZANIA: Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema maandalizi ya timu hiyo kuelekea mchezo dhidi ya JKT Tanzania yameenda vizuri, huku akitarajia ushindani mkubwa kutokana na ubora wa wapinzani wao kwenye Ligi Kuu msimu huu.

Ibenge ameeleza kuwa huu ni miongoni mwa michezo wanayoifurahia kuicheza kwa sababu ya ushindani wake mkubwa, jambo linalowapa motisha ya kufanya vizuri zaidi uwanjani.

Kwa upande wake, beki wa Azam FC, Nassor Saadun, amesema wachezaji wote wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo huo.

Mchezo huo utapigwa kesho, Aprili 17, 2026, na utakuwa LIVE kupitia #AzamSports1HD.

#NBCPL #AzamFC #JKTTanzania #AzamJKT

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *