Iran imetangaza siku ya Jumamosi, Aprili 18, kwamba imerejesha “udhibiti mkali” wa Mlango-Bahari wa Hormuz kujibu kizuizi kinachoendelea cha Marekani kwenye bandari za Iran, ikibadilisha uamuzi wake siku iliyopita wa kufungua tena njia hii ya majini ya kimkakati kwa meli za kibiashara na kuweka kivuli juu ya mazungumzo ya amani kati ya Tehran na Washington. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kamandi Kuu ya Jeshi la Iran imetangaza siku ya Jumamosi kurejesha vizuizi vyote kwenye Mlango Bahari wa Hormuz, hatua inayobadili msimamo wake iliyouchukua jana Ijumaa wa kuufungua ujia huo muhimu wa bahari.

Meli yoyote inayokaribia Hormuz “italengwa,” waonya Walinzi wa Mapinduzi wa Iran

Jeshi la wanamaji la Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, jeshi la kiitikadi la Iran, limeonya kwamba meli yoyote inayokaribia Mlango-Bahari wa kimkakati wa Hormuz “italengwa na mashambulizi” ya Tehran.

“Tunaonya kwamba hakuna chombo chochote kinachopaswa kuondoka kwenye nanga yake katika Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman. Jaribio lolote la kukaribia Mlango-Bahari wa Hormuz litachukuliwa kuwa ushirikiano na adui na chombo kinachokiuka maaizo haya kitalengwa na mashambulizi,” kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye Sepah News, tovuti ya Walinzi wa Mapinduzi.

Hapo jana Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Abbas Araghchi alitangaza kufunguliwa kikamilifu wa Mlango Bahari wa Hormuz kama sehemu mazungumzo yake na Marekani.

Tehran iliifunga njia hiyo nyembamba ya bahari inayopitisha karibu asilimia 20 ya mafuta na gesi yote asili duniani baada ya Marekani na Israel kuishambulia dola hiyo ya Uajemi mwishoni mwa mwezi Februari.

Hii leo, taarifa iliyotolewa na Kamandi Kuu ya Jeshi la nchi hiyo imesema Washington imekiuka ahadi ya kufungua kikamilifu shughuli zote za usafirishaji kupitia mlango habari huo kwa uamuzi wake wa kuendelea na mzingiro wa kijeshi iliyouweka mwanzoni mwa wiki hii.

Rais Donald Trump wa Marekani aliamuru jeshi la nchi hiyo kuweka vizuizi kwa shughuli zote za bandari za Iran ikiwa ni pamoja na kuzuia kuingia na kutoka kwa meli zinazobeba shehena ya mafuta ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *