Wajumbe wa Jumuhiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT) Mkoa wa Kilimanjaro wakiongozwa na Mwenyekiti waowamefanya ziara katika halmashauri ya Jiji la Mwanza ziara iliyokua na lengo la kujifunza na kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Jiji hilo.
Miradi iliyotembelewa na ALAT Kilimanjaro ni pamoja na Mradi wa shule ya mchepuo wa kiingereza(Nyanza English Edium)inayomilikiwa na halmashauri ya Jiji la Mwanza,Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana sambamba na hayo pia wajumbe hao wamejifunza njia bora ya ukusanyaji wa mapato kwa mfumo wa kisasa unaotumiwa na halmashauri hiyo.
Akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara yao katika Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saa Nane Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Kilimanjaro ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rombo Gilbert Tarimo amesema kuwa ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa na wamejifunza mengi ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato kwa mfumo wa kisasa,uanzishwaji wa miradi ya maendeleo nk,.
“Nichukue fursa hii kuwakaribisha wenzetu wa halmashauri ya jiji la Mwanza waje kujifunza kwetu Kilimanjaro na tuweze kubadilishana uzoefu katika uongozi lakini pia wanapota nafasi waje kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo mlima Kilimanjaro”…Alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Moshi ambaye pia ni Katibu wa ALAT Mkoa wa Kilimanjaro Shadrack Mhagama amesema kuwa wameona ni vyema kujifuza katika halmashauri nyingine ambazo zinaendelea kutekeleza majukumu mbalimbali ya kuwahudumia wananchi na kuongeza kuwa lengo kubwa ni kujifunza mbinu na jinsi ya kukabiliana na changamoto ambazo halmashauri nyingine wanapambana nazo na mafanikio wanayopata kwa kutumia mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa mapato.
Aidha katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wamejifunza namna halmashauri zinavyotekeleza miradi mbalimbali kulingana na fedha zinvyotolewa na Rais wa hawamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan sambamba na kujifunza jinsi halmashauri zinavyotoa huduma kwa wananchi zikiwepo huduma za elimu,afya nk.
“Katika Jiji la Mwanza tumeona wenzetu wamepata mafanikio mengi katika sekta mbalimbali kwani tumejionea shule ya mchepuo
(Feed generated with FetchRSS)