Watanzania wametakiwa kujiandaa na kujipanga jinsi ya kutumia fursa za matukio na mikutano mikubwa inayotarajiwa kufanyika hapa nchini ili kujiinua kiuchumi na kuongeza pato la Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji ( Mb) ameyasema hayo Jijini Arusha alipokuwa akizungumza na wadau wa utalii wanaoshiriki ufunguzi wa mafunzo ya waongoza watalii kwa lengo la kuongeza ujuzi,weledi na usalama wa wasafirishaji na wageni wanaotembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
Dkt. Kijaji amewataka wadau wa utalii hapa nchini kubuni na kuandaa vifurushi maalum vya utalii vitakavyoendana na ratiba za wageni watakaohudhuria matukio na mikutano inayotarajiwa kufanyika hapa nchi ikiwa ni pamoja na Mkutano 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2026, World Travel Awards Grand Final 2026 utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2026, pamoja na AFCON 2027, ili kuwavutia kuvitembelea vivutio vyetu.
Aidha, amewataka kuvitangaza vifurushi hivyo mapema kupitia majukwaa mbalimbali ya masoko ili kuhakikisha wageni hawa wanapata taarifa mapema kwamba wanapokuja Tanzania kuhudhuria matukio hayo, pia wana nafasi ya kipekee ya kutalii na kufurahia vivutio vya nchi yetu.
Aidha, Dkt. Kijaji ameahidi kuwa Wizara itaendelea kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi katika kuandaa mafunzo kama hayo kwa makundi mbalimbali, kwa lengo la kuongeza ujuzi na kuimarisha uwezo wa rasilimali watu, hatua itakayoiwezesha Tanzania kuendelea kushindana kwa ufanisi katika soko la kimataifa.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Nkoba Mabula amesema mafunzo hayo yamefanyika kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na TATO ikiwa ni kielelezo cha Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha sekta binafsi inakuwa jumuishi ili kukuza utalii na kuacha tabasamu kwa Watanzania.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wasafirisha watalii Tanzania (TATO) Bw. Willy Chambulo amesisitiza juu ya ukarimu, uaminifu

(Feed generated with FetchRSS)