#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe imewahukumu maofisa wawili wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Thadeus Mtui na Florian Kilango, kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tano kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni nane.

Watumishi hao walipokea fedha hizo kutoka kwa mfugaji Yuda Male kwa nyakati tofauti ili wasichukue hatua za kisheria baada ya kumkuta akilisha mifugo katika Hifadhi ya Msitu wa Chimala.

Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Daniel Mono, alieleza mahakamani kuwa washtakiwa walichukua shilingi milioni mbili mnamo Novemba 2025 na kisha milioni sita nyingine Januari 2026.

Mfugaji huyo aliamua kutoa taarifa katika vyombo vya dola baada ya kuchoshwa na usumbufu wa maofisa hao licha ya kuwa alikuwa ameshatoa kiasi hicho kikubwa cha fedha kama hongo ili aachiwe.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Irvan Msacky, mbali na kutoa adhabu ya faini, ameamuru washtakiwa hao kurejesha fedha zote milioni nane walizochukua kwa mlalamikaji.

Mahakama imesisitiza kuwa adhabu hiyo ni fundisho kwa watumishi wa umma wanaokiuka dhamana ya kulinda maliasili za nchi na badala yake kujiingiza katika vitendo vya udhalimu na hujuma dhidi ya juhudi za serikali za kuhifadhi mazingira.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *