Dar es Salaam. Kuku ndo kitu pekee ambacho kila kiungo chake kina ladha yake sasa warembo wa kizazi kipya nao wameiga ukuku kuku.

Wao kila kiungo mwilini kina pambo lake la gharama .Yaani walivyoumbwa na Mungu kwao haitoshi wanaongeza na yao

Maneno ya kuambiwa changanya na yako wao wamegeuza kwamba urembo ulioumbiwa wewe changanya na wa kwako

Kichwani kuna kusuka marasta au kuweka wigi, Asipofanya hivyo basi atataka vibanio vya nywele vidoleni kuna pete na kucha kuna rangi au kuweka za bandia

Kwenye nyonga zao siku hizi wanavaa cheni za almasi au dhahabu

Kumbuka midomoni kuna rangi zake, lip bam sijui na lip shine. Kwenye ulimi kwa ndani wanachomeka vipini flan hivi

Machoni wanabandika viini macho wao wanaita blue eyes. Sikioni kuna hereni na puani kuna kipini au hereni kama ng’ombe

Hoteli ya mtoto kuna Tanganyika jeki ya sidiria na kuchora tattoo. Mkononi kuna bangiri na saa kumbuka pia simu ya bei ghali ishikiliwe

Miguuni sasa wana mbwembwe za vile vikuku vinavyotoa akili zetu. Wanasuguliwa na kupakwa rangi ili kuvalia tusendo twa manyonya

Nilitaka kusahau kuwa shingoni pia kuna mkufu kama ile ya kwenye nyonga. Duh hadi inachosha!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *